Saturday 6 August 2016

Hirizi ya Tiffah yaibua jipya!

TIFFA2Mtoto wa Mwanamuziki Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, Tiffah Dangote
Stori: Mwandishi wetu, Risasi Jumamosi
Mtoto wa Mwanamuziki Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, Tiffah Dangote Agosti 3, mwaka huu ametimiza mwaka mmoja lakini jipya lililoibuka ni kuhusiana na dawa ‘hirizi’ aliyovalishwa mkononi na bibi yake mzaa baba, Sanura Kassim ‘Sandra’, Risasi limenyetishiwa ubuyu.
Chanzo kutoka ndani ya familia ya mastaa hao kilichoomba hifadhi ya jina lake kimedai kuwa, awali Tiffah alivishwa dawa hiyo lengo likiwa ni kumkinga na matatizo lakini Zari alipokwenda Sauzi akamvua kwa kuwa yeye si ‘muumini’ wa mambo hayo.
tiffaIkadaiwa kuwa, baada ya Zari kumvua walikaa muda mrefu bila Tiffah kuwa na ‘kadawa’ hako hali iliyomfanya mtoto huyo achelewe kutembea.
“Unajua ile dawa ina mambo mengi kwa watoto, inamsaidia kumkinga na matatizo lakini pia inamfanya atembee haraka, sasa walipoivua ikamfanya achelewe kutembea,” alisema mtoa habari huyo na kuongeza:
“Hali hiyo ilisababisha Zari na Diamond kutofautiana na mwisho wakakubaliana hirizi irejeshwe mkononi mwa Tiffah ndipo mtoto huyo alipoanza kutembea.”
Ikaelezwa kuwa, kuanza kutembea kwa Tiffah kumeibua furaha upya kwenye familia hiyo kwani walishaanza kuwa na hofu hasa ikichukuliwa kuwa, Zari ana mimba nyingine na anatarajiwa kujifungua Desemba, mwaka huu.
Kufuatia madai hayo, mwandishi wetu alimtafuta Diamond na alipopatikana alisema kuwa ni kweli mtoto wao ameanza kutembea lakini si kwa sababu ya dawa hiyo aliyofungwa mkononi.
“Hayo mambo ya kumvalisha na kumvua Tiffah ile dawa ya mkononi ni uamuzi tu lakini huwezi kusema ina uhusiano na kutembea kwake,” alisema Diamond.
speech za donald trump

Monday 30 November 2015

Obama alaani utamaduni wa ghasia za bunduki

  • 29 Novemba 2015
Image copyrightReuters
Image captionRobert Dear, mwenye umri wa miaka 57, ametajwa na watu wanaomjua kama mtu anayependa kutembea pekee yake
Rais wa Marekani Barack Obama ameshutumu utamaduni wa ghasia za bunduki baada ya watu watatu kuuawa katika shambulio lililofanywa kwenye kliniki moja ya mpango wa uzazi katika jimbo la Colorado.
Obama alisema kuwa hali hiyo imetosha sasa nchini Marekani na kuwa lazima wananchi wachukue hatua kuhakikisha kuwa watu hawapati bunduki kwa urahisi nchini humo.
Image copyrightGetty
Image captionObama asema imetosha !
Obama alisema kuwa mtu aliyefyatuliana risasi na polisi kwa saa kadhaa alikuwa akitumia bunduki ambayo kwa kawaida hutumiwa na wanajeshi.
Raia wawili na afisa mmoja wa polisi walifariki katika makabiliano hayo ingawa hadi sasa lengo la mashambulizi hayo halijulikani.
Wakati huohuo habari zaidi zimefichuka kuhusiana na mtu huyo aliyeshambulia kituo hicho cha upangaji wa uzazi.
Image captionRobert Lewis Dear aliyetekeleza mauaji huko Colorado
Robert Dear, mwenye umri wa miaka 57, ametajwa na watu wanaomjua kama mtu anayependa kutembea pekee yake na ambaye hugombana na majirani wake na polisi mara kwa mara.
Aidha polisi wanasema kuwa Robert alipiga mayowe akisema hataki kuendelea kuwepo kwa miili ya watoto akiashiria mbinu ya kuwasaidia watu kupanga familia zao.
Yamkini bwana huyo ambaye anadaiwa kuwa mtu mpweke na anapinga vikali haki ya kuavya mimba.


Saturday 26 September 2015

brand new music inamorato mtoto mremboo official video

tizama na pakua video ya msanii chipkiz omizzo inayokwenda kwa jina la inamorato,,
actually ni nyimbo ambayo imekaa poa sana na shout out ziende kwake i hope dogo atafika mbali

nilipopata chance ya kuzungumza na msanii huyu aliniambia kwambi wimbo huo ni historia ya kweli iliyomkuta katika swala zima la mapenzi,,,,

take ur tym uchek hiyo ngoma ila duh mapenzi hatareeeeee wachina hodareeeee,,,,