Monday 30 November 2015

Obama alaani utamaduni wa ghasia za bunduki

  • 29 Novemba 2015
Image copyrightReuters
Image captionRobert Dear, mwenye umri wa miaka 57, ametajwa na watu wanaomjua kama mtu anayependa kutembea pekee yake
Rais wa Marekani Barack Obama ameshutumu utamaduni wa ghasia za bunduki baada ya watu watatu kuuawa katika shambulio lililofanywa kwenye kliniki moja ya mpango wa uzazi katika jimbo la Colorado.
Obama alisema kuwa hali hiyo imetosha sasa nchini Marekani na kuwa lazima wananchi wachukue hatua kuhakikisha kuwa watu hawapati bunduki kwa urahisi nchini humo.
Image copyrightGetty
Image captionObama asema imetosha !
Obama alisema kuwa mtu aliyefyatuliana risasi na polisi kwa saa kadhaa alikuwa akitumia bunduki ambayo kwa kawaida hutumiwa na wanajeshi.
Raia wawili na afisa mmoja wa polisi walifariki katika makabiliano hayo ingawa hadi sasa lengo la mashambulizi hayo halijulikani.
Wakati huohuo habari zaidi zimefichuka kuhusiana na mtu huyo aliyeshambulia kituo hicho cha upangaji wa uzazi.
Image captionRobert Lewis Dear aliyetekeleza mauaji huko Colorado
Robert Dear, mwenye umri wa miaka 57, ametajwa na watu wanaomjua kama mtu anayependa kutembea pekee yake na ambaye hugombana na majirani wake na polisi mara kwa mara.
Aidha polisi wanasema kuwa Robert alipiga mayowe akisema hataki kuendelea kuwepo kwa miili ya watoto akiashiria mbinu ya kuwasaidia watu kupanga familia zao.
Yamkini bwana huyo ambaye anadaiwa kuwa mtu mpweke na anapinga vikali haki ya kuavya mimba.


Saturday 26 September 2015

brand new music inamorato mtoto mremboo official video

tizama na pakua video ya msanii chipkiz omizzo inayokwenda kwa jina la inamorato,,
actually ni nyimbo ambayo imekaa poa sana na shout out ziende kwake i hope dogo atafika mbali

nilipopata chance ya kuzungumza na msanii huyu aliniambia kwambi wimbo huo ni historia ya kweli iliyomkuta katika swala zima la mapenzi,,,,

take ur tym uchek hiyo ngoma ila duh mapenzi hatareeeeee wachina hodareeeee,,,,

linah no stress offisial musicvideo

bofya kutizama wimbo mpya wa lina no stress
tizama hapa video mpya ya sauti sol issabela

MANCITY CHALI,,ARSENAL NA MAN U ZAPETA

  • Saa 8 zilizopita
Image captionsanchez
Image captionTottenham
Manchester City imepoteza mechi ya pili mfulululizo huku Harry Kane akifunga bao lake la kwanza msimu huu na kuiwezesha Tottenham kutoka nyuma na kuichapa Manchester City mabao 4-1.Kevin De Bryune alianza kuifungia Manchester City huku Toby Alderweired ,Erik Lamela ,Christian Eriksen na Lamela akifunga udhia.Wakati huohuo Arsenal imeicharaza Leicester mabao 5 kwa mbili katika mechi iliochezwa kwa kasi ya hali ya juu.Alexi Sanchez aliifungia Arsenal mabao matatu huku Walcot na Giroud wakifunga bao moja kila mmoja.Manchester United nayo imepata ushindi wa mabao matatu kwa bila dhidi ya Sunderland huku Rooney ,Depay na Mata wakifunga.

KIKOSI CHA KUMLINDA RAISI CHAVUNJWA BURKINAFASO

  • 26 Septemba 2015
Image copyrightAFP
Image captionKafando
Serikali ya Burkina Faso imevunja kikosa cha kumlinda rais ambacho kiliwashika mateka mawaziri wakati wa majaribio ya mapinduzi yaliyofeli.
Hatua hiyo ilichukuliwa wakati wa mkutano wa kwanza wa serikali tangu siku ya Jumatano wakati rais wa mpito Michel Kafando aliporejeea madarakani.
Image copyrightAFP
Image captionBurkina Faso
Waziri wa masuala ya ulinzi amefutwa kazi na tume imebuniwa kuwatambua wale waliohusika katika kupanga mapinduzi hayo.
Takriban watu 19 waliuawa wakati wa maandamano ya kupinga mapinduzi hayo.

saudi arabia yakana uvumi wa vifo vya mahujaji

  • 26 Septemba 2015
Image captionMahujaji waliofariki
Saudi Arabia imekana ripoti kuwa mkanyagano uliowaua zaidi ya watu 700 karibu na mji wa Mecca ulisababishwa na kufungwa kwa barabara ili kuruhusu watu mashuhuri kuingia eneo hilo.
Wizara ya masuala ya ndani ilisema kuwa madai hayo ni ya uongo na kwamba uvumi huo ulianzishwa na vyombo vya serikali Iran ambayo ilipoteza raia 131.
Iran imeilaumu Saudi Arabia kwa mkasa na ikataka wahusika wote kuchukuliwa hatua za kisheria.

full time man city ft totenham pics za matokeo

Ligi kuu ya Uingereza Barclays Premier League imeendelea tena jumamosi ya leo tarehe 29, September – mchezo wa kwanza siku ya leo umewakutanisha Manchester City dhidi ya Tottenham Hotspur.
  Mchezo huo uliopigwa katika dimba la White Hart Lane umemalizika kwa City kupata kipigo kizito kutoka kwa Spurs.
Spurs walianza kuliona lango la Spurs katika dakika ya 25 kwa goli lilofungwa na mchezaji mpya City De Bruyne – Spurs wakafanikiwa kusawazisha dakika ya mwisho ya kipindi cha kwanza, goli likifungwa na beki wa pembeni Eric Dier.
  Dakika 5 baada ya mapumziko Spurs wakapata goli la pili lilofungwa na beki wa kati Alderweireld na muda mfupi baadae mfungaji bora wa Spurs msimu uliopita Harry Kane akafungua akaunti yake ya magoli msimu huu kwa kufunga goli la 3.
 
Dakika ya 79 Winga wa kiargentina Eric Lamela akashindilia msumari wa mwisho kwenye jeneza la City kwa kufunga goli la nne.
TIMU ZILIPANGWA HIVI
Tottenham (4-2-3-1): Lloris 7.5, Walker 6, Alderweireld 7, Vertonghen 7, Davies 6, Dier 8, Alli 6, Lamela 7 (Carroll 87), Son Heung-min 6 (N’Jie 75), Eriksen 6.5 (Chadli 68), Kane 7
Subs not used: Rose, Vorm, Trippier, Townsend, Carroll
Booked: Lamela, Dier, Eriksen, Alli, Kane   
Scorers: De Bruyne 25 
Manchester City (4-5-1): Caballero 4.5, Sagna 6, Demichelis 5, Otamendi 5.5, Kolarov 5, Fernandinho 6 (Nasri 69), Fernando 6, De Bruyne 6.5, Toure 5.5 (Jesús Navas 56), Sterling 5, Aguero 5 (Roberts 86)
Subs not used: Hart, Zabaleta, Barker, Evans
Booked: Demichelis  
Scorers: Dier 45, Alderweireld 50, Kane 61, Lamela 79 
Referee: Mark Clattenburg 4.5

ALIWATUKANA POLISI KUPITIA PAGE YAO YA FACEBOOK KILCHOFUATA KIJUE HAPA

Kila nchi ina sheria zake, Sheria za Tanzania sio lazima ziwe Sheria kwenye nchi nyingine, ukweli huo ni sawa hata kwa baadhi ya vitendo… kwa mfano kutukana polisiTanzania ni kosa kubwa kisheria na pengine ukithubutu kufanya hivyo utakumbwa na matatizo makubwa. Lakini hii kwa wenzetu wa Marekani imekaaje?
complex
Thomas Smith alikamatwa na polisi mwaka 2012 kwa kosa la kuwatukana polisi waVillage of Arena kupitia page yao ya Facebook kitendo ambacho polisi hao walidai kuwa ni kosa kubwa kisheria na hakupaswa kufanya hivyo, na kwa mujibu wa mtandao waMotherboard Thomas alipost comment kwenye page hiyo ya Facebook iliyosema…
>>> “F* ths f* cops, f* racist basturds an f* all of y’all who is racist”<<< kwenye ukurasa huo wa Facebook akiwa anajibu post iliyopandishwa kwenye page hiyo ambayo aliona imekaa kibaguzi.
arena
Mwanasheria wa Thomas alipinga madai hayo ya polisi kwa kusema kuwa hata Katibaya Marekani inamruhusu kila mtu kwa uhuru na kwa hisia kukosoa serikali na watumishi wake, na alichokifanya Thomas sio uvunjaji wa Sheria bali ni haki alionayo kikatiba!
Lakini Mahakama inachukuliaje kitendo cha kutukana polisi hata kama ni kuptia internet kwa kutumia mitandao ya kijamii? Siku ya ijumaa wiki hii Mahakama ilitoa uamuzi uliosema…
arena2
>>> “Nchi na Mahakama zimekuwa zikihifadhi haki za uhuru wa kujieleza kwa kila mtu na raia wa nchi hii, na haki hiyo haijahifadhiwa tu kwa kauli ama hotuba za heshima peke yake. Kwenye nchi hii tuna haki ya kuikosoa serikali na watumishi wake kwa hisia. Utumiaji wa baadhi ya maneno haiondoi haki hiyo wala kugeuza kitendo hicho kuwa kinyume na sheria. Tunatumaini kuwa Arena Police Department na department nyingine za Polisi  kwenye majimbo tofauti wataelewa suala hili.”<<< nukuu kutoka kwenye blog ya Aquino Law Firm iliyokuwa inasimamia kesi ya Thomas Smith.
Thomas Smith sasa yupo huru kuendelea na maisha yake akiwa hana kosa lolote huku kituo hicho cha polisi kimeambiwa kimlipe kijana huyo fidia ya dola 35,000 kwa kumpotezea muda ambayo kwa pesa ya Tanzania tunazungumia fidia ya Tzs milioni 80,500,000!

wasanii wanaoingiza mkwanja mrefu africa ya mashariki hawa apa


Ni good news ndani ya nchi nyingine staa wenu wa muziki anafanya poa… kiukweli tumeusikiliza SANA muziki toka nje ya TZ sasa ni time yetu kuteka headlines kwenye nchi zao pia.
Kwenye stori kubwa Kenya iko pia hii ya list ya wanamuziki wanaoingiza pesa nyingi kwa sasa Kenya, list ambayo imepata baraka ya MCSK na KECOBO ambao ni wasimamizi wa hakimiliki nchini Kenya.
Hawa ni wanamuziki wa Kenya wanaoingiza pesa nyingi zaidi.
1.Sauti Sol
2.Bahati
3.Lady Wanja
4.Willy Paul
5.Mum Cherop
6.H-Art the Band
7.Gloria Muliro
8.Rabbit ‘King Kaka’
9.John De Mathew
10.Hellena Ken
Hii ni list ya jumla ya wakali wanaoingiza pesa nyingi zaidi 
1. Diamond (Tanzania)
2.Sauti Sol
3. Christina Shusho (Tanzania)
4. Alikiba (Tanzania)
  1. Bahati
  2. Lady Wanja
7. Jose Chameleon
8. Rose Mhando (Tanzania)

baraza la sanaa tanzania basata limeufungia rasmi wimbo wa viva roma soma hapa

wimbo mpya wa roma umefungiwa rasmi


barasa la sanaa tanzania basati limeufungia rasmi wimbo mpya wa msanii wa hip hop tanzania roma mkatoliki uitwao viva roma

BASATA wamesema sababu kubwa ya kuufungia wimbo huo ni kwamba hakuna ushahidi wa mambo yote yalioandikwa ndani ya wimbo huo

baada ya  taarifa ya kuungia wimbo huo roma alipost instagram screenshot ya taarifa hiyo na kuandika

   ''life is not fair!!!!TUNAKUFA MASIKINI KWA KUWATETEA WANYANG'ANYI!!!!!!!!
eeh mungu baba wa mbinguni nisaidie
viva roma
viva roma
viva roma

saa chache baada ya wimbo huo kutoka septemba 9 2015 rapper huyo aliandika kupitia ukurasa wake wa instagrama kua ametishiwa kufungiwa wimbo wake

''wanataka kuufungia wimbo wangu kisa tu nimeongea ukweli''
akaongeza na kusema ''inaniuma sana natamani hata kulia nikiona ukweli haupewi nafasi''

source;john amani