Saturday 26 September 2015

saudi arabia yakana uvumi wa vifo vya mahujaji

  • 26 Septemba 2015
Image captionMahujaji waliofariki
Saudi Arabia imekana ripoti kuwa mkanyagano uliowaua zaidi ya watu 700 karibu na mji wa Mecca ulisababishwa na kufungwa kwa barabara ili kuruhusu watu mashuhuri kuingia eneo hilo.
Wizara ya masuala ya ndani ilisema kuwa madai hayo ni ya uongo na kwamba uvumi huo ulianzishwa na vyombo vya serikali Iran ambayo ilipoteza raia 131.
Iran imeilaumu Saudi Arabia kwa mkasa na ikataka wahusika wote kuchukuliwa hatua za kisheria.

No comments:

Post a Comment